Imani Yetu


Karibu

Ibada Zetu

Huduma Zetu

Mahali Tulipo

Kusudi Letu

Imani Yetu

Uongozi Wetu

Wamisionari
Wetu

Wasiliana Nasi

Niambie Zaidi
Juu Ya Wokovu!

English

 

IMANI YETU

KUHUSU MUNGU
Twamwamini Mungu mmoja, wa milele, aliye muumba na mtawala wa ulimwengu, aliye nafsi tatu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
Mwanzo 1:1; Zaburi 90:2; Mathayo 28:19; Yohana 10:30; 1 Petro 1:2; Warumi 8:9-11; 2 Wakorintho 13:14
Rejea

KUHUSU YESU KRISTO
Twaamini kwamba Yesu Kristo alizaliwa na bikira Mariamu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, na kwamba Yeye ni Mungu kweli na mwanadamu kweli. Twaamini kwamba Bwana Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu akiwa dhabihu kamili kwa dhambi zetu. Alizikwa, akafufuka siku ya tatu akishinda mauti na dhambi. Akapaa mbinguni mahali aliko mkono wa kuume wa Mungu, naye atarudi duniani ili kutawala kama Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme.
Mathayo 1:18-25; Isaya 9:6; Yohana 1:1-5; 14:10-30; Waebrania 4:14,15; 1 Wakorintho 15:1-4; 2 Wakorintho 5:21; Warumi 1:3,4; Matendo 1:9-11; 1 Timotheo 6:14,15; Tito 2:13;
1 Petro 1:18,19; 2:24
Rejea

KUHUSU ROHO MTAKATIFU
Twaamini kwamba Roho Mtakatifu ni mmoja na Mungu Baba na Mwana wa Mungu. Aingia kila Mkristo dakika ile amwaminipo Yesu Kristo. Anawapa Wakristo nguvu na ufahamu wa mambo ya kiroho, na kuongoza Mkristo katika njia ya haki. Anampa kila Mkristo kipawa cha kutumia katika kanisa. Kama Wakristo tunapaswa kuenenda chini ya utawala wake kila siku.
Warumi 8:9; 2 Wakorintho 3:17; Yohana 16:7-13; 14:16,17; Matendo 1:8; Waefeso 1:13,14; 4:30; 5:18, Wagalatia 5:25; 1 Wathesalonike 5:19
Rejea

KUHUSU BIBLIA
Twaamini kwamba Biblia ni Neno la Mungu kwetu sisi. Iliandikwa na waandishi wanadamu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Twaamini kwamba Biblia yenyewe ndiyo hiyo iliyo kuu na inayopasa kukubaliwa na watu wote katika imani na maisha. Kwa sababu ni yenye pumzi ya Mungu, Biblia ni kweli tupu, bila mchanganyiko wowote wa kosa.
2 Timotheo 3:16,17; 2 Petro 1:20,21; 2 Timotheo 1:13; Zaburi 119:105,160; Mithali 30:5
Rejea

KUHUSU WANADAMU
Twaamini kwamba mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu, kusudi afanane na Mungu na tabia zake. Mwanadamu aliumbwa na Mungu ili kutawala viumbe vyote na kumletea Mungu sifa na utukufu. Twaamini kwamba mwanadamu alimwasi Mungu akitaka kujitawala, na hali hiyo ya uasi na kuepa utawala wa Mungu inaitwa dhambi. Hali hiyo ya dhambi ndiyo inayowatenga wanadamu na Mungu na kumletea mwanadamu shida za maishani mwake.
Mwanzo 1:27; 2:17; Zaburi 8:3-6; 51:5; 58:3; Warumi 1:20; 3:23; 5:12-21
Rejea

KUHUSU WOKOVU, KARAMA YA MUNGU
Wokovu ni zawadi ya Mungu kwetu sisi, lakini lazima tupokee zawadi h iyo. Haiwezekani kujipatia zawadi hiyo kwa njia ya matendo mema wala yoyote tunayoweza kufanya sisi, bali inawezekana kwa njia moja tu, kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa kumwamini Yesu Kristo na kukubali kwamba Yeye alijitoa kwa ajili ya dhambi zetu, ndivyo tunavyoweza kusamehewa na kuokolewa na adhabu ya dhambi. Tukiamua kuacha nia ya kujitawala na kumgeukia Yesu katika imani, sisi tunaokolewa. Wokovu huo tunaopata ni wa milele na huanza papo hapo tunapomkubali Yesu kama Mwokozi.
Yohana 1:12; 3:3; 5:24; 14:6; Warumi 6:23; 5:1; Wagalatia 3:24-26; Waefeso 2:8,9;
1 Yohana 5:13
Rejea

KUHUSU UZIMA WA MILELE
Kwa sababu uzima tunaopata katika Yesu Kristo ni wa milele, mwaamini anaweza kuwa na uhakika na wokovu siku zote. Baada ya kuokoka haiwezekani kamwe kupotea tena. Wokovu ni jambo alilotenda Mungu kwa nguvu zake na neema zake, kwa hivyo si kwa nguvu za mwaamini anavyoweza kuendelea na wokovu. Ni kwa nguvu na neema za Mungu na hivyo tunao uhakika kwamba wokovu wetu ni wa milele kama Biblia inavyosema.
Yohana 10:29; 2 Timotheo 1:12; Waebrania 7:25; 10:10,14; 1 Petro 1:3-5
Rejea

KUHUSU MAMBO YAJAYO
Watu waliumbwa na Mungu ili kuishi milele. Baada ya maisha haya na kuaga dunia tutaendelea kuishi. Aidha tutaishi tukiwa tumetengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi, ama tutaishi pamoja na Mungu hata milele, kwa sababu ya msamaha wa dhambi na wokovu katika Kristo. Kwa hao wasiookoka watakwenda mahali palipoitwa Jehanum. Kwa hao waliookoka watakwenda kuishi mahali palipoitwa Mbinguni.
Yohana 3:16,36; Yohana 14:17; Warumi 6:23; Warumi 8:17-18; Ufunuo 20:15;
1 Wakorintho 2:7-9
Rejea

 
 

Updated 03 May 2008